Monday, April 22, 2013

VIJANA WA KIISLAMU WASHAURIWA KUHUSU SUALA ZIMA LA NDOA.

Vijana wa kiislamu wake kwa waume wameshauriwa kuliendea suala zima la ndoa,ushauri huo umetolewa katika kongamano la mabinti wa kiislamu lililowashikirisha mabinti mbalimbali wa kiislam wanaosoma katika vyuo mbali mbali hapa jijini Mwanza.
Hoja kuu katika kongamano hilo ilikuwa suala zima la ndoa, katika mada hii waliongelea masuala mbali mbali kama, maana ya ndoa, misingi ya ndoa , mambo ya kuangalia wakati wa kuchagua mchumba na mengine mengi.

     Aidha walieleza maana ya ndoa , kuwa ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliwekwa na jamii.Ndoa ya kiislamu (Nikah) ni mkataba (Aqd) wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya kiislamu.

  Katika uslamu ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kutokana na umuhimu wake  katika kujenga na na  kuiendeleza jamii.Ndoa katika mtazamo wa Uislamu ina umuhumu sana katika jamii kama , Kuihifadhi jamii na maradhi, kuihifadhi jamii na zinaa, kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri, Utulivu wa moyo,mwili  na akili, kujenga mapenzi , huruma  na ushirikiano katika familia na faida nyingine nyingi ambazo mja anaweza kuzipata wakati akiwa ameshiriki katika ibada hii kwa kufuta utaratibu uliowekwa na kuelekezwa katika sheria za Uislamu.

    Waislamu wameshariwa wawe makini katika kuchagua mchumba , na katika suala hili wameshauriwa  kuwa wachague wachumba ambao wana sifa mbali mbali za kumpendeza Allah na miongoni mwa sifa hizo ni, Dini(Uislam), Tabia njema, Rika, Elimu na suala zima la kizazi.
  Jambo la muhimu ambalo limesisitizwa sana miongoni mwa sifa ni suala zima la dini na kila muislamu ni wajibu alizingatie  kwa hakika dini ni  kigezo kikubwa cha mwanzo muislamu yoyote anatakiwa azingatie kwa mujibu wa mtume wetu Muhammadi (s. a.w), kuhusu kipengele hiki cha dini katika kuchagua mchumba , tunafahamishwa katika hadidhi kuwa:

        Abu Hurairah ameeleza: kuwa Mtume(s .a. w) amesema :
                " Mwanamke anaolewa kwa vitu vine: Kwa utajiri wake, Kwa ujuzi wake, Kwa uzuri wake  na kwa dini yake .Mchague yule mwenye msimamo mzuri wa dini..." (Bukhari na Muslim)

Hivyo shime alaiku ndugu zangu waislamu tuwe  makini katika kuchagua wachumba na kuindea ibada nzima ya ndoa kama ilivyowekwa wazi katika sheria za dini yetu  na pia kufuata amri za Allah zilizowekwa wazi kwetu na Mtume (s. a. w)

Wednesday, April 17, 2013

TANGAZO LA KONGAMANO LA WANAWAKE

 ASSALAM ALAYKUM.NDUGU KATIKA IMANI MNAALIKWA KWNYE KONGAMANO LA WANAVYUO LINALO WAJUMUISHA WANAWAKE WA KIISLAM WA VYUO MBALIMBALI VYA JIJI LA MWANZA.
MAHALI:   SAUT
UKUMBI:   M1
MUDA:      SAA 3:00 ASUBUHI HADI 7:00 MCHANA
          MADA MBALIMBALI ZITATOLEWA NA MIJADALA KATIKA MADA HIZO
          TUNAOMBA MJUZE MWENZAKO PINDI UPATAPO TAARIFA HII
    WABILLAH TAWFIQ

Wednesday, April 10, 2013

MAJINA YA WAHITIMU WALIO KAMILISHA FEDHA ZA VYETI.



ST. AUGUSTINE UNIVERSITY OF TANZANIA
                           MWANZA
MAJINA YA WAHITIMU WALIO KAMILISHA FEDHA ZA VYETI.
v ADVANCED DIPLOMA IN ACCOUNTANCY
1.    JOHARI RAMADHANI
2.    HADIJA MASHAMU
3.    ZAUJATI CHAMBO
4.    KHALFANI.N.MSANGI
v ADVANCED DIPLOMA IN PROCUREMENT AND LOGISTICS MANAGEMENT
1.    MOHAMED. R. MWAJA
v BACHELOR OF ARTS IN PUBLIC RELATION AND MARKETING
1.  BARKA AHMED
2.  SHEILA MSUYA
3.  MGOJA BAKARI
4.  CHAUREMBO.M.ALLY
v BACHELOR OF BUSINESS ADMINISTRATION
1.     MOHAMEDI. A. MOHAMEDI
2.     KHALIDI MAHADI
3.      HASHIMU ZUBERI
4.     MOHAMED. A. MBADJO
v BACHELOR OF ARTS IN SOCIOLOGY
1.     REHEMA .H. KITWE
2.     PILI MAZIGE
v BACHELOR OF SCIENCE IN PROCUREMENT AND SUPPLY CHAIN MANAGEMENT
1.     MWANAIDI DUMWALLAH
2.     SEIF .A. MUYO
3.     SALMA .I.MBEO
4.     ZAITUNI LEMA
           
v BACHELOR OF PHILOSOPHY WITH EDUCATION
1.     AYOUB . A.KENGWA
2.     ASHA .H. ALLY
v BACHELOR OF LAWS
1.     HEMED SMITH
v BACHELOR OF ARTS IN MASS COMMUNICATION

v BACHELOR OF ARTS IN ECONOMICS
       1. MBAROUK MATATA
v BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION
1.     SAADA .J. RAMADHANI
2.     MUNIRA .E. MALLYA
3.     RAMADHANI THOMAS
4.     HALIMA NASSORO MULIKA
5.     KHARIFA  .A.MTABUZI
6.     NUHU .J.SAID
7.     HALIMA  ABDILLAH
8.     FAUZU .I. KINOBE
9.     IZADINI. H. HATIBU
10.                        ILOZE NGEREZA
11.                        RAJABU SHABAN SALLA
12.                        SHABANI. A. ALLI
13.                        ABDARAHMANI. R.HONDO
14.                        MAPELE ALLY
15.                        OMARY MACHETA
16.                        ALLY FERUZI
17.                        AISHA STAMBULI
18.                        MWAJUMA SALEHE
19.                        ADHA .H.ABDILLAH
20.                        ZUHURA  ZENGWA
21.                        ANYIMIKE THOMSON MWAKYANJALA(Muhitimu mwaka 2011 cheti kimepotea)
22.                        JAMILAH
           
NB.
v JINA LA KOZI YA MUHITIMU

Monday, May 7, 2012

TANGAZO LA MAHAFALI YA MKOA TAMSYA MWANZA KWA NGAZI YA VYUO VIKUU

A.ALAYKUM,NDUGU KATIKA IMANI,Mnaalikwa katika mahafali yatakayo fanyika ktk chuo cha mtakatifu augustino SAUT Mwanza,siku ya tarehe 20.05.2012 hivyo mnaombwa kushirikiana kwa hali na mali kwa wale si wahitimu kwa kuchangia kiaasi cha sh 4000/=.

Tuesday, February 14, 2012

VALENTINE DAY

Valentine day ni siku ya WAPENDANAO au siku ya WAZINZI?
Kwa muislam kushiriki katika sikukuu ya wapendahao ni sawa na kukataa yale yote alokujanayo MTUME(S.A.W)kwani chimbuko la siku ya wapendanao ni kinyume na mafundisho ya UISLAM.

Saturday, January 14, 2012

EDA NA MAAMRISHO YAKE.

ﻢﻴﺣﺮﻟﺍ ﻦﻤﺣﺮﻟﺍ ﻪﻠﻟﺍ ﻢﺴﺑ Eda ni kipindi anachokaa mwanamke aliyeachika au aliyefiwa na mumewe, na baada ya kipindi hicho ndoa yake huwa halali. Na imeitwa eda kwa jina hili kutokana na jina la kiarabu ‘iddah’ kwa kukusanya kwake (idadi) ya miezi au ‘quruu’ [1] au hedhi au vipindi vya tohara ya hedhi. HEKIMA YA KUHALALISHWA EDA Hapa tunaona baadhi ya mawazo ya wanachuoni ambao wameona hizi ndizo hekima au sababu za kuwekewa eda shari'ah, ingawa hekima ya mwanzo na ya mwisho ni hiyo ya mwisho hapo chini ya fungu hili: Kutambua kama mwanamke ni mjamzito au la. Kuweza kubainika nasaba au kizazi ili kuepusha utata wa kutokujulikana nani ndiye baba. Kipindi ambacho mke anakaa eda kiwe kifupi au kirefu kinaangaza mwangaza wa kweli kuhusu uzito wa ndoa yao
na mkataba mtakatifu walioufunga baina yao. Eda ya kufiwa inamwezesha
mwanamke kutoa huzuni zake na kupata muda wa kujiliwaza na msiba uliomtokea wa kipenzi chake. Pia inamhifadhi kwa kutokuwa chombo cha kusemwa na kuzungumzwa kila apitapo. Kupata nafasi mume na mke kutafakari kwa makini kuhusu mahusiano yao kabla hawajavunja muungano wao wa kifamilia na haswa katika
talaqa ivunjikayo (ya kwanza au ya pili) Ama HEKIMA ya juu kuliko
zote kuhusu eda ni UTIIFU kwa maamrisho ya Mola wetu (Subhaanahu Wa Ta'ala). Kwani kuna wengi wanaotoa hoja za akilini mwao kama vile kudai kuwa siku hizi kuna
utaalam wa kujua kama mwanamke ana mimba kwa vipimo bila haja ya kukaa eda mwanamke n.k. Hoja kama hiyo si ya busara maana ni sawa na kusema ‘siku hizi kuna kinga za mimba kama kondomu n.k, kwa hiyo zinaa iwe halali!’ Wamesahau kuwa HEKIMA kuu ni UTIIFU kwa Muumba na Utekelezaji wa MAAMRISHO yake na mengine ni ya ziada na wala si ya msingi. Mwenyeezi Mungu Anatujua zaidi kuliko tujijuavyo nafsi zetu. HUKUMU ZA EDA 1- Eda Kisheria Kishari'ah eda ina maana nyingi, mojawapo: Kupata yakini kwa kile kiumbe chenye kuzaliwa ili kuepukana na mchanganyiko wa nasaba. Na vilevile eda hekima yake hiyo eda ni kutoa fursa na muda kwa mume na mke baada ya talaka huenda kwa
kipindi hicho wakamaliza tofauti zao na kurudiana na kuishi tena kama wanandoa kamili. Na pia sababu nyingine ni kulipa na kutekeleza haki haki zote za mume aliyefariki (ikiwa ni eda ya kufiwa) na kudhihirisha athari za kumpoteza mume, kwa kipindi cha maombolezi, nako ni kujizuia huyo mwenye eda na kujipamba, kujiremba n.k. kama tutakavyoona mbele. Na eda ni wajibu kwa mwanamke wakati anapoachana na mumewe, ima kwa talaka au kwa kufiwa na mumewe au ‘faskh’ (kutenguka kwa ndoa) au ‘khulu’u’ [2] (kujivua na ndoa hiyo). Na ni sharti awe ashaingiliwa na mumewe. Na eda haiwi kwa mwanamme, na anaruhusiwa kuoa mwanamke mwingine bila hata kusubiri kwisha hiyo eda ya mkewe. Ila tu kama kutakuwa na kizuizi, kama kutaka kumuoa dada ya mkewe, maana hairuhusiwi kishari'ah kuchanganya baina ya dada wawili kwa wakati mmoja kwani kishari'ah atakuwa yule mke aliyempa talaka ni wake hadi atakapomaliza muda wa eda yake. Au pia kama ana wake wanne na amempa talaka mmoja kati yao, haitoruhusiwa kwake kuoa mwanamke mwingine hadi eda ya huyo aliyemuacha imalizike vilevile. Kishari'ah hairuhusiwi kuwa na zaidi ya wake wanne. 2- Kumalizika Eda Kunatofautiana muda wa kwisha eda kutokana na sababu au aina za eda yenyewe. Aina zenyewe ni hizi zifuatazo: 1. Eda ya aliyepewa talaka: Ni ‘quruu’ (vipindi vya hedhi/tohara) tatu, endapo atakuwa keshaingiliwa na mumewe na hakuwa ni mwenye mimba, au aliyekoma hedhi, au mdogo asiyepata hedhi bado. Na haya yamefafanuliwa na Mwenyeezi Mungu (Subhaanahu Wa Ta'ala) Aliposema: {{Na wanawake walioachwa wasubiri (wasiolewe) mpaka Twahara tatu ziishe…}} Al-Baqarah: 228 2. Eda ya aliyefiwa na mumewe: Ni miezi minne na siku kumi, kama alivyoipangia Mwenyeezi
Mungu katika Qur-aan: {{Na wale wanaofishwa (wanaokufa) miongoni mwenu na kuacha wake; hawa (wake) wasubiri (wasiolewe) miezi minne na siku kumi.}} Al- Baqarah: 234. Kiwango hiki ni endapo atakuwa si mjamzito (mwenye mimba), ama akiwa ni mjamzito basi eda yake itakwisha pale atakapojifungua. Kama tutakavyoeleza zaidi hapo mbele. Hakuna tofauti ya huyu aliyefiwa ikiwa mumewe alimwingilia alipokuwa hai au hakumwingilia, yote ni mamoja. Na atakapokufa mume na hali mkewe yuko katika eda ya talaqa rejea, itageuka eda hiyo na kuwa ni eda ya kufiwa. Ila endapo mume wa mke aliyeachwa talaka wazi atakuwa amekufa, na kumuacha kwake kulikuwa wakati akiwa na afya yake nzuri au kwa matakwa ya mwanamke mwenyewe, basi katika hali hiyo mke atakamilisha tu hiyo eda ya talaka na hatokaa eda ya kufiwa. 3. Eda ya aliyekoma hedhi: (Kwa kupindukia miaka) Ni miezi mitatu kama Alivyosema Mwenyeezi Mungu: {{Na wale waliokoma kutoka hedhi miongoni mwa wake zenu, ikiwa mnayo shaka (katika muda wao wa eda), basi muda wao wa eda ni miezi mitatu…}} At-Twalaaq: 4. Na itakapowarejelea hedhi wakati ashaanza eda yake, basi atakaa eda ya ‘quruu’ badala ya miezi. Ama akiwa amepata hedhi mara moja au mbili tu kisha akawa katika hedhi yake iliyokoma basi arejee kwenye kukaa eda ya miezi mitatu badala ya ‘quruu’. 4. Eda ya mjamzito (mwenye mimba): Inamalizika kwa kujifungua kama Anavyosema hapa Mwenyeezi Mungu (Subhaanahu Wa Ta'ala). : {{…na wanawake wenye mimba eda yao ni mpaka watakapozaa.}} At- Twalaaq: 4. Ama ikiwa mwanamke eda yake ishaanza naye hajui kama ana mimba na baadaye ikadhihiri hiyo mimba, basi atabadili eda yake kutoka kuwa ni eda ya ya mwezi na kuwa ni eda ya mimba (ujauzito). Na ataendelea na eda hadi atakapojifungua. 5. Eda ya msichana ambaye hajafikia kupata hedhi, na
eda ya mwanamke aliyevunja ungo ambaye pia hajawahi kupata hedhi na ambaye hakufikia umri wa kukoma hedhi: Hawa wote eda yao ni miezi mitatu kutokana na ushahidi wa maneno Yake Allaah: {{Na wale waliokoma kutoka hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka (katika muda wao wa eda), basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, na (ndio muda wa eda kwa wale) ambao hawajapata hedhi
bado.}} At-Twalaaq: 4. Lakini endapo itamtokezea hedhi mmoja kati ya wanawake wa aina hiyo kabla ya kumalizika muda wa eda yake, ataibadili hiyo eda na kuwa ni ya ‘quruu’ badala ya ile ya miezi iliyokuwa mwanzo. 6. Eda ya mwanamke aliyezaa mapacha au zaidi: Itaanza baada ya kumzaa pacha wa mwisho, kwani mazingatio katika eda ya ujauzito ni kujulikana kiumbe (bara-atu rahim), kwa kuondokana kabisa na ujauzito. 7. Eda ya aliyetowekewa na mumewe: Aliyetoweka ni yule ambaye hajulikani alipo na habari zake hazikusikika tangu alipoondoka au kutoweka pamoja na kutafutwa kwa muda mrefu. Wanachuoni wa shari'ah
wametenganisha kati ya kupotea kwake kwa aina
mbili: kujulikana alipo na kutojulikana. Ikiwa alipo panajulikana na ikiwa yuko salama huko alipo ima kibiashara, kikazi au kimatembezi, na kukakatika habari zake, basi wamesema wanachuoni kuwa ndoa yao bado itabaki hadi kuthibitike mauti yake au atoe talaqa au kupite muda mrefu ambao si wa kawaida ya yeye kupotea hivyo. Ikifikia hali hiyo, basi mke atakaa eda na kisha itakuwa halali kwake kuolewa tena. Ama ikiwa kupotea kwake kutajulikana kama vile kumesikika kuwa ndege aliyopanda katika safari yake imeanguka na hakupona mtu au gari alilosafiria limepinduka n.k, hapo mke atakaa eda
ya mfiwa ya miezi minne
na siku kumi. Na ikiwa kupotea kwake kumekuwa kurefu mno na hajulikani kama kapatwa na nini, na kukawa hakuna mawasiliano ya aina yoyote, basi hapo mke atasubiri kipindi cha miaka minne kisha atakaa eda ya mfiwa ya miezi minne na siku kumi. Ila ni vizuri zaidi kabla ya hivyo kuwe kumefanyika majuhudi makubwa ya kumtafuta kwa kutumia njia za kila aina na haswa kwa wakati huu ambapo njia za mawasiliano zimekuwa nyingi na nyepesi mno. Ni vizuri kutolewe taarifa kwenye
vyombo vya habari, mitandao, mabalozi n.k. Lakini ikiwa kutoweka kwa bwana kukawa hatimaye kumebainika alipo na kukawa na mawasiliano, mathalan kumejulikana kuwa yuko jela na kifungo chake ni miaka mingi, au kasafiri mbali na atakawia sana kurudi, hapo kutatazamwa kama muda huo mrefu utamuathiri mke na watoto wake ima kiuchumi au kimwili au kiusalama, basi hapo mke ana haki ya kusubiri au kudai talaqa au kuomba kuachishwa na mume huyo. Qaadhi au Shaykh au Imaam au kiongozi wa dini ataangalia sababu za pande zote na dharura iliyopo kabla ya kumwachanisha mke na mumewe. 3- Yanayopaswa Kwa Mwenye Eda Wanachuoni wengi wa kishari'ah wamekubaliana kuwa mwenye eda anapaswa kukaa katika nyumba ya ndoa kwa muda wa eda yake yote hadi itakapomalizika. Ikiwa eda hiyo ni ya talaqa au ya kuomba kuachwa (kuachishwa) au ya kifo, haitakikani atoke ila kwa haja maalum au nyudhuru za kishari'ah la sivyo atakuwa ametenda dhambi. Na mume anaweza kumkataza asitoke
ikiwa eda hiyo ni ya talaka, na mrithi ana haki ya kumzuia kutoka ikiwa eda hiyo ni ya kufiwa. Ila baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa katika eda ya kufiwa mke anakaa eda yake atakavyo. Na inapaswa kwa mwenye eda ya kufiwa akae katika maombolezi (al-ihdaad) kwa
muda wote wa eda yake. Na kuomboleza ni kuacha yeye kujipamba kwa mavazi ya marembo rembo, kuvaa dhahabu, na kujipaka manukato n.k. Kufanya hivyo kuna maana ya kuchunga na kuheshimu ule uhusiano wa kindoa uliokuwa baina yake na mumewe, nako pia ni kuonyesha utiifu kwa uhusiano wao. Pia kunapatikana katika huo muda wa maombelezi, utulivu wa nafsi ya mwanamke na kufikiria maisha mapya ya ndoa yamkabiliyo mbeleni. MAMBO MBALIMBALI KATIKA EDA NA HASWA EDA YA KUFIWA Haya ni baadhi ya mambo ambayo ni haramu kwa mwenye eda kuyafanya kishari'ah: Kujitia manukato mwilini au nguoni. Kujitia rangi za mdomo, rangi za kucha, poda, na aina zote za vipodozi. Kujitia wanja wa macho bila dharura ya kuumwa. Kuvaa nguo za rangi rangi: au ya rangi moja lakini yenye kuvutia na yenye mapambo. Si lazima hata hivyo kuvaa kaniki kama inavyodhaniwa na wengi au shuka la bafta n.k. Kuvaa mapambo ya dhahabu, fedha, lulu, almasi na madini mengine, ikiwa ni pete, mkufu, hereni, bangili na vinginevyo. Kujitia hina popote maungoni
panapoonekana na watu. Kutoka nje pasipo na dharura. Haikatazwi mwenye eda kutoka nje kama hana wa kumtegemea kwa mahitaji yake, mathalan ikiwa inambidi kufanya kazi kwa kupata mahitaji yake, kwenda kununua mahitaji yake ya nyumbani, au kufundisha kama mwalim n.k. Kuolewa Kuposwa MAMBO YA UZUSHI YANAYOFANYWA NA WAKAA EDA Kuna mambo yafanywayo na baadhi ya wanawake wenye kukaa eda ambayo ni
ya kijahili na hayapo katika mafunzo ya dini yetu hii nyepesi. Mambo hayo ima kwa kutokujua hao wayafanyao, au kwa kufundishwa na maustaadh na masheikh wababaishaji. Utakuta baadhi ya wenye eda hawawezi kutoka majumbani mwao sharti wawe wametoka na fimbo au bakora, wengine wakitoka huku wamevaa matambara kama mwendawazimu, na wengine ambao hawajistiri inavyopasa utawaona nywele zao hawazichani wala kuzisafisha kwani wameambiwa hairuhusiwi kuchana wala kuoga kila mara. Hadi mwanamke akimaliza eda yake, si chawa na uvundo unaotoka mwilini mwake kwa kutojisafisha kila mara. Hayo ni matunda ya mafunzo ya waalimu wa dini wasio na elimu sahihi ya kutegemewa. Haya ni baadhi ya mambo ya uzushi katika eda yaliyokuwa yakifanyika zamani na yanayofanyika hadi sasa katika jamii yetu: Kuja mtu kama mwalimu au Sheikh kumnuiza huyo mwenye eda wakati aanzapo eda yake, na kumchagulia saa ya kuianza hiyo eda. (Eda huanza pale tu akatapo roho mume. Hakutakikani kunuizwa wala kungojea saa maalum ya kuianza). Baadhi ya wenye eda huwa na khofu na eda na kuamini kuwa ikiwa hajakaa hiyo eda ipasavyo, basi atafikwa na balaa au wazimu au kifo. Kutonyanyua sauti ili isisikike na watu walio nje. Si vizuri mwanamke kunyanyua sauti yake lakini kwenye hili kunakuwa kunatiliwa mkazo mno hata inakuwa vigumu watu kumsikia, hata kama anahitaji kitu au anamuhitaji mtu amjie, matokeo yake anakuwa kama bubu au yuko kifungoni hata baadhi ya mahitajio yake anayakosa kwa kuamini kuwa hapaswi kutoa sauti. Kupelekwa chooni kwa kuchukuliwa vyetezo vya ubani, na yeye kubeba fimbo ya mumewe au kisu au kukamata kaa la moto lililozimika, au ndimu, au chumvi. Wengine hawaendi chooni usiku kwa kuamini
ni vibaya na huwa wanawekewa chombo chumbani cha kujisaidia haja zake. Matokeo chumba kinakuwa hakitamaniki na kuhatarisha pia afya ya mkazi. Hata akiwa faragha hawezi kutoa kitambaa cha kichwa akiamini kuwa ni balaa. Kwa maana amefundishwa kuwa akifanya hivyo atatoa nafasi ya wazimu kumuingia kichwani mwake. Kutoruhusiwa kulalia kitanda chenye godoro na badala yake alalie kitanda cha kamba au mbao kisicho na tandiko juu yake au jamvini. Kuvaa aina fulani ya viatu
tu, kama vya mbao na sharti visimtoke mguuni. Na wanaamini kuwa kiatu kikimvuka tu basi na wazimu umemvaa saa hiyo hiyo. Kukatazwa kuonana na wanaume hata kama ni maharimu wake. Kutoruhusiwa kusema na mtu tokea alasiri ya siku ya Alkhamiys tena baada ya kuogeshwa! Hadi mshuko wa siku ifuatayo ya Ijumaa. Hata akitokewa na hatari hawezi kupiga yowe la kuhitaji msaada! Kulazimishwa kufunga Swawm siku hizo za Alkhamyis na Ijumaa na kusoma Qur-aan na nyiradi ndefu ndefu. Haijulikani kama Swawm hiyo ni ya eda au ya nini, na wala haijulikani ilipofundishwa. Kuja kusomewa kila Alkhamiys na huyo mwenye kumsomea hupewa chochote. Naam, hayo ndiyo hao masheikh wababishaji
wayafundishayo ili waweze kupata chochote. Na mambo mengi ya dini yamezushwa ili kuwanufaisha hao wayaanzishayo. M.Mungu awaongoze. Kukatazwa hata kujitazama katika kioo kwa muda wa eda yake yote. Kutoamkia au kutoamkiwa kwa kupewa salaam kama kuambiwa ‘anakusalimu fulani’ bali huambiwa ‘Fulani anakupeni hujambo?’ Kutojibu neno lolote katika hali ya kusimama. Ila ni sharti akitaka kumjibu mtu, apige magoti ndipo ajibu. Kulalia kitu kinachomhusu
marehemu chini ya mto. Au kulalia ndimu, msumari na wembe. Kutokukata kucha za mikono wala za miguu kwa muda wote huo wa eda wa miezi minne na siku kumi. Nako ni kufuga uchafu na kujihatarisha yeye mwenyewe kujidhuru kwa makucha yake. Kuzikusanya nywele zote zilizong’ooka ili ziende zikatupwe mbali kabisa kama baharini siku atokapo eda yake pamoja nywele anyolewazo siku hiyo. Kuondoshwa hiyo eda katika sehemu za pwani, kwa kuchagua siku maalum na kwenda kuosha nguo pwani na kugonga madebe na vyuma na kukaa siku tatu bila kuonekana na watu. Haya ni mambo yaliyokuwa yakifanywa zamani na mengine hadi leo yanaendelea kufanyika katika baadhi ya jamii yetu kutokana na kudanganywa watu na pia kwa kutokuelewa wengi wetu na kwa kutofanya jitihada za kujielimisha. Alhamdulillah hivi sasa kutokana na kwamba elimu sahihi imeenea sehemu nyingi na wengi wanasoma, basi mambo hayo yamepungua sana. Mambo yote yaliyopo hapo juu, mengi ni ya kusikitisha na mengine ni ya kuihusisha dini yetu na ugumu na kuipa picha mbaya kabisa. Mwenyeezi Mungu Anasema: {{…wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini}} Al-Hajj: 78 Pia Anasema vilevile: {{… Mwenyeezi Mungu Anakutakieni mepesi wala hawatakieni magumu}} Al- Baqarah: 185 Vilevile tumeona mifano mingi ambayo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisisitiza kuhusu kutotia uzito na ugumu katika dini. Alikuwa akisema: ‘‘Nimeletwa kufundisha dini ya Uislam iliyo nyepesi’’ Pia alipowatuma ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) na Muadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwenda Yemen, aliwausia kufanya wepesi kwa kuwabashiria kheri watu wa huko na kuwavuta katika dini kwa upole bila kuwatilia uzito na kuwakimbiza. Sasa ni ajabu kuona baadhi ya Masheikh wakiwafundisha watu mambo magumu magumu na yasiyokuwa hata katika mafundisho ya dini yetu hii nyepesi. Mwenyeezi Mungu Atujaalie hima ya kujifunza na kutafuta elimu ya haki na iliyo sahihi, na atuepushe na uzushi na ya batili. [1] Quruu: Kuna kutofautiana kwa maoni ya wanachuoni kuhusu hii ‘quruu’, je, ni Twahara au ni hedhi? TOFAUTI YA MAULAMAA JUU YA QURUU Quruu, ni neno linalotumika kwa maana ya hedhi au Twahara kwa vile linaoana na maana zote mbili. Hanafi na Hanbali, wanaona kwamba neno hili lina maana ya hedhi. Hii inamaanisha kwamba mwanamke aliyeachwa atakaa hadi hedhi tatu zimalizike. Ikiwa hedhi itakatika baada ya mara moja tu, basi itakamilishwa na miezi. Ama Ma-Imaam Maalik na Ash-Shaafi'iy, wao wanaona
kwamba neno hili lina maana ya Twahara. Na Twahara hapa ni vile vipindi vinavyokuwa baina ya hedhi mbili. [2] Khul'u: Kilugha: Ni neno lenye asili ya Kiarabu lenye kumaanisha kuondosha na kuvua. Ni kama vile mtu anavyoivua nguo kuitoa mwilini. Kishari'ah: Ni kukiondosha kifungo cha ndoa kwa tamko la kuvua au kwa tamko lingine lenye maana kama hiyo kwa mkabala wa mali anayoitoa mke kumlipa mumewe. Na hili bila shaka limeruhusiwa ili kumpa mwanamke uhuru wa kujiengua toka kwenye ndoa na mumewe baada ya maisha kwa upande wake kufikia ukomo wa kutoweza
tena kuishi kwa raha na mumewe. Dalili yake: Ni Aayah ya 229 ya Surat Al-Baqarah, Mwenyeezi Mungu Anasema: {{Talaka (unazoweza kumrejea mwanamke) ni (zile zilizotolewa) mara mbili (za kwanza). Kisha ni kumweka kwa wema au kumwacha kwa ihsani (Wala usiweze kumrejea tena mpaka aolewe na mume mwengine maadam ametimiza mara tatu katika kumwacha ukimrejea). Wala si halali kwenu kuchukua chochote mlichowapa (wake zenu), isipokuwa (wote wawili wakiogopa ya kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyeezi Mungu, hapo itakuwa hapana dhambi kwao (mwanamme wala mwanamke katika) kupokea
(au kutoa) ajikomboleacho mwanamke.
Hii ndio mipaka ya Mwenyeezi Mungu; basi msiiruke. Na watakaoivuka mipaka ya Mwenyeezi Mungu, hao ndio madhalimu (wa nafsi zao) }}. Ama kwenye Hadiyth ni kile kisa cha mke wa Thaabit bin Qays aliyekwenda kushtaki kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya mumewe, pamoja na kuwa mumewe hakuwa na tatizo la dini wala tabia bali yeye hakumpenda na akawa
anakhofia kutotekeleza wajibu wake kama mke. Mtume aliwatenganisha lakini kwa kumtaka mke airejeshe bustani/shamba aliyokuwa amepewa na mumewe kama ni mahari. Hadithi hiyo ipo katika Swahiyh Al-Bukhaariy 5273

Thursday, January 12, 2012

MASHARTI YA HIJABU YA KISHERIA

Assalam alaykum baada ya kumhimidi ALLAH Tabaaraka wataala na kumtakia rehma mtume Muhammad swallallahu alayhi wassalam leo katika kukumbushana tutaja masharti nane [8]ya hijabu ya kisheria tukisemama hijabu ya kisheria tunamaanisha ALLAH anaikubali na kuiridhia na endapo moja katika masharti hayo yakipungua[ hata moja] basi hijabu haikubaliki mbeleya ALLAH na mvaaji ataadhibiwa sikuya qiyama[1]kwanza kabisa inatakiwa isitirimwili mzima[ikihusisha uso pamoja na miguu namikono][2]jalabibi hilo halitkiwi kuwa namapambo yeyote [3]kitambaa kitakachotumikakinatakiwa kiwekizito kisiwe chepesi chenye kuonyesha ndani [4]guo hilolinatakiwa kuwa pana lisiwe lenye kubana[5]halitakiwikuwa namanukato -na tunapenda kutiliamkazo hapa kwani wanawake wengi hupuuza nuktahii[6]halitakiwikufanana na mavaziya kikafiri[7]halitakiwi lifanane namavazi yakiume[8]halitakiwi liwe ni vazi la fakhari hivyo nawausia mama zangu nadada zangu kujitahidi kuzifanyia kazi sharti hizo ili ALLAH tabaaraka wataala aweze kuzikubali