Monday, April 22, 2013

VIJANA WA KIISLAMU WASHAURIWA KUHUSU SUALA ZIMA LA NDOA.

Vijana wa kiislamu wake kwa waume wameshauriwa kuliendea suala zima la ndoa,ushauri huo umetolewa katika kongamano la mabinti wa kiislamu lililowashikirisha mabinti mbalimbali wa kiislam wanaosoma katika vyuo mbali mbali hapa jijini Mwanza.
Hoja kuu katika kongamano hilo ilikuwa suala zima la ndoa, katika mada hii waliongelea masuala mbali mbali kama, maana ya ndoa, misingi ya ndoa , mambo ya kuangalia wakati wa kuchagua mchumba na mengine mengi.

     Aidha walieleza maana ya ndoa , kuwa ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliwekwa na jamii.Ndoa ya kiislamu (Nikah) ni mkataba (Aqd) wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya kiislamu.

  Katika uslamu ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kutokana na umuhimu wake  katika kujenga na na  kuiendeleza jamii.Ndoa katika mtazamo wa Uislamu ina umuhumu sana katika jamii kama , Kuihifadhi jamii na maradhi, kuihifadhi jamii na zinaa, kuendeleza kizazi kwa utaratibu mzuri, Utulivu wa moyo,mwili  na akili, kujenga mapenzi , huruma  na ushirikiano katika familia na faida nyingine nyingi ambazo mja anaweza kuzipata wakati akiwa ameshiriki katika ibada hii kwa kufuta utaratibu uliowekwa na kuelekezwa katika sheria za Uislamu.

    Waislamu wameshariwa wawe makini katika kuchagua mchumba , na katika suala hili wameshauriwa  kuwa wachague wachumba ambao wana sifa mbali mbali za kumpendeza Allah na miongoni mwa sifa hizo ni, Dini(Uislam), Tabia njema, Rika, Elimu na suala zima la kizazi.
  Jambo la muhimu ambalo limesisitizwa sana miongoni mwa sifa ni suala zima la dini na kila muislamu ni wajibu alizingatie  kwa hakika dini ni  kigezo kikubwa cha mwanzo muislamu yoyote anatakiwa azingatie kwa mujibu wa mtume wetu Muhammadi (s. a.w), kuhusu kipengele hiki cha dini katika kuchagua mchumba , tunafahamishwa katika hadidhi kuwa:

        Abu Hurairah ameeleza: kuwa Mtume(s .a. w) amesema :
                " Mwanamke anaolewa kwa vitu vine: Kwa utajiri wake, Kwa ujuzi wake, Kwa uzuri wake  na kwa dini yake .Mchague yule mwenye msimamo mzuri wa dini..." (Bukhari na Muslim)

Hivyo shime alaiku ndugu zangu waislamu tuwe  makini katika kuchagua wachumba na kuindea ibada nzima ya ndoa kama ilivyowekwa wazi katika sheria za dini yetu  na pia kufuata amri za Allah zilizowekwa wazi kwetu na Mtume (s. a. w)

1 comment:

  1. Maasha-Allah Naona maemdeleo ya blog ni mazuri,kikubwa jitahidini kuweka post mpya angalau Hata kwa wiki maramoja. Vyakupost ni vingi mfano khutba za ijumaa na matokeo mbalimbali.

    ReplyDelete

Tafadhali tumia lugha nzuri na yenye staha katika kutoa maoni yako,kwani lugha chafu hazitavumiliwa,hivyo basi kuwa mstaarabu.Mwenyezi Mungu na akuongoze.Aamin!