Sunday, December 18, 2011

SAMUCO WACHAGUA VIONGOZI WAPYA.

VIONGOZI WAPYA SAMUCO. Safu
mpya ya uongozi ya samuco leo
tarehe 18.12.2011
wamechaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika ukumbi
wa M1. Amir ni Ngeleza Iloze (BAED2). Naibu Amir ni Said
Muhana(BAED1). Katibu ni
Mbarouk Matata(BAEC2) na
Naibu katibu ni Mbaraka Said
(ADA1). Amirat ni Hadija
Shaaban(LLB2) na Naibu Amirat ni Husna Kimolo(BAED1).
Mweka hazina ni Mwajabu
Mashaka(LLB3) na msaidizi
wake ni Aisha Stambuli
(BAED2). Hii ndio safu
nzima.Inshaallah tuwape ushirikiano ili waweze kufanya
kazi zao vizuri.

Tuesday, December 13, 2011

UHARAMU WA KUJITOA MANII KWA MKONO[masturbation]

  1. Assalam alaykum warahmatullah wabarakaatuh inshaALLAH leo katika mlango wa kukumbushana tutakuwa tukizungumzia kadhia ya masturbation au 'punyeto'kwanza kabisa tufahamu maana ya masturbation;ni mtu kutumia mikono yake au kifaa chochote kile na kutumia tupu yake kwa lengo la lakujistarehesha kitendo hichi kwa hakika ni haramu kwa ushahidi wa aya ambayo inapatikana katika sura almuuminuun aya ya5-6[na wale wanaohifadhi tupu zao isipokuwa kwa wake zao au kwa wale iliyomilikimikono yao ya kuume[mateka ;watumwa]kwao haitakuwa lawama[yaani hawatolaumiwa kukidhi haja zao zakimatamaniokwao wao]kwahiyo namna yeyote ile ya kukidhi matamanio isiyokuwa yamke au wale waliyomilikiwa kama tulivyotaja ni HARAMU katika hili inaingia masturbation vilevile ukirejea tafsiir ibn kathiir amenukuu kauli ya imamu shafi kuwa yeye imam shafi ametumia aya hiyo katika kueleza uharamu wa masturbation pia rejea fatawa ya shaykh fawzaan mujeledi wa4 uk 272 fatwa namba 277pia rejea fataawa ya shaykh albani fatwa namba 56.

Sunday, December 4, 2011

MIAKA HAMSINI YA UHURU

sisi kama Waislamu ipo haja yakuliangalia suala hili la kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru katika mtizamo mwingine kabisa.
Abdulwahid sykes(2002),anasema katika kitabu chake"Historia iliyofichwa kuhusu harakati za waislamu dhidi ya ukoloni wa mwingereza katika Tanganyika"kuwa wakati wa utawala wa Julias K. Nyerere rais wa Tanzania mamabo matatu yaliakuawa ni mwiko kuyaeleza: kuwa historia ya kudai uhuru wa Tanganyika ilianza kabla yake,pili waislamu ndio walikuwa katika harakati za kupambana na ukoloni,tatu kutokana na historia ya kudai uhuru waioslamu walikuwa na kinyongongo na serikali kwa kutothamini mchango wao na kutotekeleza ahadi iliyoweka wakati wa kudai uhuru.
Tunajua kuwa serikari yetu haina dini kabisa lakini wananchi wake wanadini na wanao uhuru na haki ya kuwabudu, sasa kutokana na mchango wa waislamu kutoonekana katika nchi hii ilo tumelizoea ila hatufurahi kuona tunashelekea miaka 50 ya uhuru wakati serikali inayotambua uwepo wadini kwa waunanchi wake imeshidwa kabisa kuwaruhusu waislamu kuwa na mahakama ya kadh pamaja na mambo mengine,sisi waislamu tunathamini sana pepo kuliko kitu kingine. Tunajiuliza hasa nini kinacho zorotesha jambo hili, sisi waislamu tunamini mahakama ya Qadh ni moja ya haki yao si yakuimba wala kuidai bali itekelezwe mara moja, kama yalivyo tekelezwa mambo mengine kama kurusiwa kuvaa hijab kwa wanafunzi mashuleni, ,masomo ya dini na kufanya ibada nyingine. kuna watu wanadhani kuwa maisha ya dunia ndio basi tu kuyaishi wanatumia pesa nyingi kunufaisha matumbo yao na kusahau kuwa "UNAWEZA KUTUMIA FEDHA NYINGI KUNUNUA DUNIA ILA UWEZI KUTUMIA FEDHA HIYO KUNUNUA PEPO"

Friday, December 2, 2011

WASOMI WAFAHAMISHENI WAISLAM KATIBA- KABEKE.

Mkurugenzi wa radio ya Kiislam radio Iqra fm 100.0 ya jijini Mwanza Ustadh Kabeke akizungumza na waislam wasomi wa chuo kikuu cha Mt. Augustine (SAUT) cha jijini Mwanza baada ya sala ya Ijumaa jana.Ustadh Kabeke aliwaasa wasomi hao kutokana na uelewa wao wa mambo mbalimbali ya kijamii,hivyo kuwataka kuwaelimisha waislam juu ya katiba,kwani wapo waislam ambao hawajui kilichomo ndani ya katiba inayotumika sasa hivyo hata mchakato wa katiba mpya hawajui wajadili nini kwani hata rangi ya katiba ya zamani hawaijui,hivyo jukumu la kuwaelimisha ni la wajuzi ambao ni wasomi. Pia ustadh Kabeke aliwataka hususan wale wanaosomea sheria kuwa msaada mkubwa juu ya suala hili. Kwani ni ukweli uliowazi kuwa vikundi na madhehebu ya dini yanatakiwa kushiriki katika mchakato wa katiba mpya hivyo ni lazima waislam wawe na uelewa wa kutosha ili iwe rahisi kutoa michango yao juu ya katiba mpya iliyokwenye mchakato.

Tuesday, November 22, 2011

Mashallaaaaah!Ng'ombe akichinjwa kwaajili ya kitoweo siku ya Eid Elhajj.Nyama iliandaliwa na wanajumuiya walifaidi pamoja na watoto yatima pia watu wa karibu walipata mgao ili nao washerehekee Eid Elhajj kwa furaha.
Nyama ikiandaliwa kwa waajili ya kuigawa kwa jumuiya ya watu wanaozunguka jumuiya ya chuo cha SAUT wakati wa sherehe ya Eid Elhajj mwaka 2011.Hakika ilikuwa siku ya furaha kubwa kwa wana SAMUCO.Mashallaaaaah.

Monday, November 21, 2011

Waislam wakisikiliza kwa umakini wa hali ya juu mada iliyokuwa ikwasilishwa katika ukumbi wa M1 katika chuo cha SAUT.
Mlezi pamoja na viongozi.Picha hii ilipigwa baada ya mahafali ya kuwaaga wahitimu wa mwaka 2010.
Sherehe na kumbukumbu.Wahitimu wamependeza.
Ustadh Hussein ambaye sasa anachukua masters akiwahutubia waislam katika ukumbi wa M11.
Mlezi wa SAMUCO Ndg.Altaf Hirani Mansoor akitoa hotuba kwa waislam chuo cha SAUT.
Amir wa TAMSYA mkoa Ndg.Ahmed Binde pamoja na naibu Amir wa TAMSYA Mkoa wa Mwanza Ndg.Abdul-Rasul Maheta wakimsindikiza mlezi Ndg.Altaf Hirani.

Amir wa TAMSYA akisoma risala ya wahitimu kwa mgeni rasmi.
Mlezi akimkabidhi katibu mhitimu zawadi.
Ndg.Altaf Hirani akiwa anapitia risala ya wahitimu kwa umakini mkubwa.
Mlezi wa SAMUCO akitoa msaada kwa mlezi mwakilishi wa kituo cha watoto yatima.
Mlezi wa SAMUCO akizungumza jambo na Rais wa TAMSYA katika mahafali iliyo fanyika chuo cha SAUT.
Rais wa TAMSYA akisikiliza linaloendelea katika ukumbi akiwa makini kabisa sambamba na mlezi wa SAMUCO katika mahafali ya kuwaaga wahitimu wa mwaka 2010 yaliyofanyika katika chuo cha SAUT kwenye ukumbi wa M11 mwaka2010.

Maamiri wastaafu kutoka SAUT na CBE wakisoma shairi katika mahafari ya kuwaaga wahitimu wa mwaka 2010.
Mlezi wa SAMUCO Ndg.Altaf Hirani akihojiwa na kituo cha ITV baada ya mahafali ya kuwaaga wahitimu wa Kiislam wa mwaka 2010 katika chuo cha SAUT.
Kina dada wa vyuo mbalimbali vya Mwanza wakiwa makini kusikiliza mada katika kongamano lililofanyika kaika ukumbi wa M1 chuo cha SAUT.

Friday, November 18, 2011


Katibu mkuu wa SAMUCO akitoa maelekezo wakati wa kugawa misaada kwa watoto yatima wa kituo cha Upendo Daima wakati wa mahafali2010.

Ndg.Altaf Hirani Mansoor akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa mwakajana 2010.

Mlezi wa SAMUCO Altaf Hirani akitafakari jambo wakati wa kongamano lililofanyika ukumbi wa M1 SAUT.

Wanajumuia wakiume wa SAUT wakiwa na makamu mkuu wa chuo kikuu cha SAUT Mwanza Rev. Dr.Charles Kitima na mlezi Altaf Hirani.

Rev.Dr.Kitima akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wa jumuia ya samuco pamoja na mlezi wa samuco Altaf Hilani katika msikiti wa SAUT Mwanza

Tuesday, November 15, 2011

Dr.Kitima na mlezi wa SAMUCO Ndg.Altaf Hirani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vingozi.
Dr.Kitima vice chanceler wa saut akishirikiana na jumuiya ya SAMUCO kutoa misaada kwa yatima.
Mlezi Ndg.Altaf Hirani akipanda mti huku akitizamwa kwa karibu na katbu Bw.Abdulrasul Maheta.
Katibu wa SAMUCO Bw.Abdulrasul akikagua ujenzi wa upanuzi wa msikiti wa SAUT.
Katibu wa SAMUCO Bw.Abdu-rasul Maheta akitazama ujenzi wa sehemu ya kutawadhia katika msikiti wa SAUT.
Amiri wa SAMUCO Ndg.Makame Ally akipanda mti katika kuhifadhi mazingira.

Mlezi wa SAMUCO Ndg.Altaf Hirani akipiga picha ya pamoja na watoto yatima.
Mlezi wa SAMUCO Ndg.Altaf Hirani akitoa maelekezo kwa makatibu Abdul-rasul Maheta na Mbarouk Matata juu ya upanuzi wa msikiti na jumuiya ya SAMUCO.

MWANAFUNZI AJINYONGA CHUO CHA SAUT.

Mwanafunzi wa sheria mwaka wa kwanza katika chuo cha Mt.Augustine campus ya Mwanza amejinyonga hadi kufa.Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea siku ya jumamosi tarehe 12/11/2011,wanasimulia kuwa walimkuta mwanafunzi huyo akiwa ananing'inia juu ya mti nyuma ya maktaba ya chuo.Histori ya mwanafunzi huyo mkimya wa sheria inasemekana tabia yake hiyo ya ukimya ndio iliyomponza.Kwani inaelezwa kuwa jamaa huyo kutoka Mkoa wa Kilimanjaro alikuwa hana muda wa kuzungumza na wenzake,hivyo wanafunzi wa karibu yake ambao analala nao chumba kimoja cha bweni walianza kumchokoza ili azungumze.Wakaamua kumtengenezea kashfa mbaya ya ushoga ambapo kila wakati walikuwa wakimwita shoga kitendo ambacho kilimuudhi marehemu.Habari za yeye kuwa shoga zilienea na kumfikia rafiki yake wa kike ambapo naye alimwambia ajijue kivyake kwani yeye hawezi kuwa na mwanaume wa namna hiyo.Kibaya zaidi ni kuwa watu wa karibu ndio walienda kwa binti huyo na kumwambia rafiki yake ni shoga.Lengo lao ilikuwa wamuudhi ili azungumze tu lakini ikashindikana na marehemu akafikia uamuzi mzito wa kujinyonga.Marehemu aliacha ujumbe wa sababu za yeye kujinyonga na kuwataja wote waliomtengenezea kashfa hiyo chafu.Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Kilimanjaro kwaajili ya maziko.Matukio ya kujinyonga chuo cha SAUT yamekuwa yakiripotiwa mara kadhaa.Innalillah Wa inna Ilayh Rajiuun.

Friday, November 11, 2011

WANAWAKE WASOMI WA KIISLAM KUFANYA KONGAMANO KUBWA KESHO.

Wanawake wa kiislam ambao ni wasomi kutoka vyuo vikuu jijini Mwanza kufanya kongamano kubwa katika ukumbi wa M3 uliopo Malimbe katika chuo kikuu cha Mt.Augustino-SAUT.Kongamano hilo litawakutanisha wasomi wanawake kutoka katika vyuo mbalimbali vya jiji la Mwanza.Mada zitakazo jadiliwa ni pamoja na Haki Ya Mwanamke Kwa Mumewe,Kupenda Ni Nini?Kwa Mtazamo wa Uislam na mengineyo yanayohusu Wanawake.Wahadhiri katika kongamano hilo ni Shekhat Zabibu kutoka Mwanza na wengine kutoka Mombasa,Kenya.Hivyo Waislam wote kinadada na kinamama mnakaribishwa sana.

Sunday, November 6, 2011

WAISLAM SAUT WAKISHEREHEKEA EID EL-HAJI.

Swala ya eid el-haji iliswaliwa kwenye msikiti wa chuo na kuswalishwa na Sheikh Hassan Kabeke ambaye ni maarufu jijini Mwanza.Kwakuwa eid el-haji ni eid ya kuchinja,hivyo Ng'ombe alichinjwa na nyama kugawiwa swadaka kwa jumuiya inayozunguka chuo cha St.Augustine.Pia jumuiya ya wanachuo wakiislam walishiriki na watoto yatima wa kituo cha Upendo Daima kilichopo Malimbe.Mbali ya kushiriki na watoto hao pia watoto hao walipewa vitu mbalimbali kama mafuta,sabuni,mchele na mbuzi mmoja.Vitu hivyo vilikabidhiwa na makamu mkuu wa chuo (vc)Father Charles Kitima.Jumuiya ya Waislam pia walisherehekea eid kwa kupanda miti mia moja na tatu,mitatu ikiwa ya matunda na mingine ya kawaida wakiongozwa na makamu mkuu wa chuo Dr.Kitime pamoja na mlezi mkuu wa jumuiya ya waislamu SAMUCO ndugu Altf Hirani.

Tuesday, November 1, 2011




Katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa M1 Jumapili ya tarehe 30/10 katika chuo cha Mt.Augustine(SAUT) cha jijini Mwanza.Kongamano lilikuwa maalum kwa kuwakaribisha mwaka wa kwanza,na kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo vyote vya Mwanza. Vyuo vilivyoshiriki ni pamoja na wenyeji SAUT,CUHAS,BUTIMBA,FISHARIES,Ukiliguru,CBE,VETA na vyuo vingine jirani.Mashekh waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na Ust.Ilunga Kapungu(picha no2) pamoja na Ust.Hassan Kabeke(picha no3).Mashekhe wakiwaasa wasomi hao kwa ujumla kuacha kubadili tabia pindi wanapofika vyuoni na kuacha maadili ya Uislam.Kwani wengi wakifika vyuoni hawataki kujulikana kama wao ni waislam.Pia walitoa wito kwa wasomi mara wanapohimu kwenda kuzisaidia taasisi za kiislam badala ya kukaa pembeni na kulaum pindi mambo yanapokwenda kombo. Waislam pia wameaswa kuunganisha tabaka mbili zilizopo za walio na elimu ya mazingira na elimu ya dini.

Saturday, October 29, 2011

WAISLAM NIDHAMU NZURI CHUO CHA SAUT-FR.KITIMA


Father Kitima ambaye ni makamu mkuu wa chuo(VC) cha Mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza( St.Augustine University of Tanzania)- SAUT ameridhishwa na nidhamu inayooneshwa na Waislam katika chuo hicho."Kwakweli tangu nikabidhiwe chuo hiki kikiwa na wanachuo wapatao 300 na hadi sasa 13,000,cha kushangaza jinsi Waislam wanavyoongezeka nidhamu nayo inazidi kuongezeka,nawapongeza kwa hilo"alisema Father Kitima.Aliongeza kuwa anayofuraha kuwa na wanafunzi wa kiislam katika chuo cha SAUT lakini akaonya juu za siasa kali ndani za jumuia ya waislam chuoni hapo kwa kusema "hata katika kanisa katoliki siasa kali zipo".Alizungumza hayo wakati akiongea na viongozi wa jumuiya ya waislam saut(SAMUCO) akiwa ofisini kwake,ambapo katika kikao hicho alitoa ruhusa ya upanuzi wa msikiti chuoni hapo.SAMUCO ilifikia hatua ya kuamua kupanua msikiti kutokana na idadi ya Waislam kuongezeka mwaka hadi mwaka hivyo msikiti kuwa mdogo na kuwalazimu wengine kusalia nje kwenye jua na inapotokea mvua wakati wa sala wengine hulazimika kulowa. Upanuzi huu kukamilika unahitaji kiasi cha Tsh milion mbili,hivyo tunatoa wito kwa yoyote atakaye guswa kwani nguvu za wanajumuiya zimeisha kutokana na michango mingi na majukumu mengine yanayohitaji fedha na ukizingatia wengi hutegemea mkopo,hivyo jumuiya inawaomba kujitolea.

Friday, October 28, 2011

UPANUZI WA MSIKITI CHUO CHA SAUT-MWANZA

Harakati za upanuzi wa msikiti unaoendea kufanyika katika msikiti wa chuo cha mtakatifu Agustino Mwanza Tanzania.Hivyo tunaomba kwa mtu yeyote kujitolea kwa chochote ilikuweza kufanikisha upanuzi huu.

Saturday, October 22, 2011

KARIBUNI SANA KWENYE BLOG HII.

Kwanza nimshukuru Allah(s.w) kwa kuwezesha kuwepo kwa blog hii.Pia nimtakie rehma na amani mtume wetu Muhammad(s.a.w) na waja wema wote tangu Adam hadi kiama. Blog hii ni yetu sote hivyo tunakaribisha habari,makala mbalimbali na uchambuzi.Kama unamaoni, makala au habari tutumie e-mail www.sautmuslims21@gmail.com. Ndugu zanguni jukumu la kuelimisha umma ni letu sote hivyo tusaidiane kuuondoa umma katika maovu na kuupeleka katika wema. Karibuni sana kwenye blog hii wote. Uislam ni kitu kimoja!

ASSALAAM-ALEYKUM NDUGU WAISLAM.