
Father Kitima ambaye ni makamu mkuu wa chuo(VC) cha Mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza( St.Augustine University of Tanzania)- SAUT ameridhishwa na nidhamu inayooneshwa na Waislam katika chuo hicho."Kwakweli tangu nikabidhiwe chuo hiki kikiwa na wanachuo wapatao 300 na hadi sasa 13,000,cha kushangaza jinsi Waislam wanavyoongezeka nidhamu nayo inazidi kuongezeka,nawapongeza kwa hilo"alisema Father Kitima.Aliongeza kuwa anayofuraha kuwa na wanafunzi wa kiislam katika chuo cha SAUT lakini akaonya juu za siasa kali ndani za jumuia ya waislam chuoni hapo kwa kusema "hata katika kanisa katoliki siasa kali zipo".Alizungumza hayo wakati akiongea na viongozi wa jumuiya ya waislam saut(SAMUCO) akiwa ofisini kwake,ambapo katika kikao hicho alitoa ruhusa ya upanuzi wa msikiti chuoni hapo.SAMUCO ilifikia hatua ya kuamua kupanua msikiti kutokana na idadi ya Waislam kuongezeka mwaka hadi mwaka hivyo msikiti kuwa mdogo na kuwalazimu wengine kusalia nje kwenye jua na inapotokea mvua wakati wa sala wengine hulazimika kulowa. Upanuzi huu kukamilika unahitaji kiasi cha Tsh milion mbili,hivyo tunatoa wito kwa yoyote atakaye guswa kwani nguvu za wanajumuiya zimeisha kutokana na michango mingi na majukumu mengine yanayohitaji fedha na ukizingatia wengi hutegemea mkopo,hivyo jumuiya inawaomba kujitolea.