Tuesday, November 22, 2011
Monday, November 21, 2011
Friday, November 18, 2011
Tuesday, November 15, 2011
MWANAFUNZI AJINYONGA CHUO CHA SAUT.
Mwanafunzi wa sheria mwaka wa kwanza katika chuo cha Mt.Augustine campus ya Mwanza amejinyonga hadi kufa.Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea siku ya jumamosi tarehe 12/11/2011,wanasimulia kuwa walimkuta mwanafunzi huyo akiwa ananing'inia juu ya mti nyuma ya maktaba ya chuo.Histori ya mwanafunzi huyo mkimya wa sheria inasemekana tabia yake hiyo ya ukimya ndio iliyomponza.Kwani inaelezwa kuwa jamaa huyo kutoka Mkoa wa Kilimanjaro alikuwa hana muda wa kuzungumza na wenzake,hivyo wanafunzi wa karibu yake ambao analala nao chumba kimoja cha bweni walianza kumchokoza ili azungumze.Wakaamua kumtengenezea kashfa mbaya ya ushoga ambapo kila wakati walikuwa wakimwita shoga kitendo ambacho kilimuudhi marehemu.Habari za yeye kuwa shoga zilienea na kumfikia rafiki yake wa kike ambapo naye alimwambia ajijue kivyake kwani yeye hawezi kuwa na mwanaume wa namna hiyo.Kibaya zaidi ni kuwa watu wa karibu ndio walienda kwa binti huyo na kumwambia rafiki yake ni shoga.Lengo lao ilikuwa wamuudhi ili azungumze tu lakini ikashindikana na marehemu akafikia uamuzi mzito wa kujinyonga.Marehemu aliacha ujumbe wa sababu za yeye kujinyonga na kuwataja wote waliomtengenezea kashfa hiyo chafu.Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Kilimanjaro kwaajili ya maziko.Matukio ya kujinyonga chuo cha SAUT yamekuwa yakiripotiwa mara kadhaa.Innalillah Wa inna Ilayh Rajiuun.
Friday, November 11, 2011
WANAWAKE WASOMI WA KIISLAM KUFANYA KONGAMANO KUBWA KESHO.
Wanawake wa kiislam ambao ni wasomi kutoka vyuo vikuu jijini Mwanza kufanya kongamano kubwa katika ukumbi wa M3 uliopo Malimbe katika chuo kikuu cha Mt.Augustino-SAUT.Kongamano hilo litawakutanisha wasomi wanawake kutoka katika vyuo mbalimbali vya jiji la Mwanza.Mada zitakazo jadiliwa ni pamoja na Haki Ya Mwanamke Kwa Mumewe,Kupenda Ni Nini?Kwa Mtazamo wa Uislam na mengineyo yanayohusu Wanawake.Wahadhiri katika kongamano hilo ni Shekhat Zabibu kutoka Mwanza na wengine kutoka Mombasa,Kenya.Hivyo Waislam wote kinadada na kinamama mnakaribishwa sana.
Sunday, November 6, 2011
WAISLAM SAUT WAKISHEREHEKEA EID EL-HAJI.
Swala ya eid el-haji iliswaliwa kwenye msikiti wa chuo na kuswalishwa na Sheikh Hassan Kabeke ambaye ni maarufu jijini Mwanza.Kwakuwa eid el-haji ni eid ya kuchinja,hivyo Ng'ombe alichinjwa na nyama kugawiwa swadaka kwa jumuiya inayozunguka chuo cha St.Augustine.Pia jumuiya ya wanachuo wakiislam walishiriki na watoto yatima wa kituo cha Upendo Daima kilichopo Malimbe.Mbali ya kushiriki na watoto hao pia watoto hao walipewa vitu mbalimbali kama mafuta,sabuni,mchele na mbuzi mmoja.Vitu hivyo vilikabidhiwa na makamu mkuu wa chuo (vc)Father Charles Kitima.Jumuiya ya Waislam pia walisherehekea eid kwa kupanda miti mia moja na tatu,mitatu ikiwa ya matunda na mingine ya kawaida wakiongozwa na makamu mkuu wa chuo Dr.Kitime pamoja na mlezi mkuu wa jumuiya ya waislamu SAMUCO ndugu Altf Hirani.
Tuesday, November 1, 2011



Katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa M1 Jumapili ya tarehe 30/10 katika chuo cha Mt.Augustine(SAUT) cha jijini Mwanza.Kongamano lilikuwa maalum kwa kuwakaribisha mwaka wa kwanza,na kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo vyote vya Mwanza. Vyuo vilivyoshiriki ni pamoja na wenyeji SAUT,CUHAS,BUTIMBA,FISHARIES,Ukiliguru,CBE,VETA na vyuo vingine jirani.Mashekh waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na Ust.Ilunga Kapungu(picha no2) pamoja na Ust.Hassan Kabeke(picha no3).Mashekhe wakiwaasa wasomi hao kwa ujumla kuacha kubadili tabia pindi wanapofika vyuoni na kuacha maadili ya Uislam.Kwani wengi wakifika vyuoni hawataki kujulikana kama wao ni waislam.Pia walitoa wito kwa wasomi mara wanapohimu kwenda kuzisaidia taasisi za kiislam badala ya kukaa pembeni na kulaum pindi mambo yanapokwenda kombo. Waislam pia wameaswa kuunganisha tabaka mbili zilizopo za walio na elimu ya mazingira na elimu ya dini.
Subscribe to:
Posts (Atom)