Tuesday, November 15, 2011
MWANAFUNZI AJINYONGA CHUO CHA SAUT.
Mwanafunzi wa sheria mwaka wa kwanza katika chuo cha Mt.Augustine campus ya Mwanza amejinyonga hadi kufa.Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea siku ya jumamosi tarehe 12/11/2011,wanasimulia kuwa walimkuta mwanafunzi huyo akiwa ananing'inia juu ya mti nyuma ya maktaba ya chuo.Histori ya mwanafunzi huyo mkimya wa sheria inasemekana tabia yake hiyo ya ukimya ndio iliyomponza.Kwani inaelezwa kuwa jamaa huyo kutoka Mkoa wa Kilimanjaro alikuwa hana muda wa kuzungumza na wenzake,hivyo wanafunzi wa karibu yake ambao analala nao chumba kimoja cha bweni walianza kumchokoza ili azungumze.Wakaamua kumtengenezea kashfa mbaya ya ushoga ambapo kila wakati walikuwa wakimwita shoga kitendo ambacho kilimuudhi marehemu.Habari za yeye kuwa shoga zilienea na kumfikia rafiki yake wa kike ambapo naye alimwambia ajijue kivyake kwani yeye hawezi kuwa na mwanaume wa namna hiyo.Kibaya zaidi ni kuwa watu wa karibu ndio walienda kwa binti huyo na kumwambia rafiki yake ni shoga.Lengo lao ilikuwa wamuudhi ili azungumze tu lakini ikashindikana na marehemu akafikia uamuzi mzito wa kujinyonga.Marehemu aliacha ujumbe wa sababu za yeye kujinyonga na kuwataja wote waliomtengenezea kashfa hiyo chafu.Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda Kilimanjaro kwaajili ya maziko.Matukio ya kujinyonga chuo cha SAUT yamekuwa yakiripotiwa mara kadhaa.Innalillah Wa inna Ilayh Rajiuun.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Tafadhali tumia lugha nzuri na yenye staha katika kutoa maoni yako,kwani lugha chafu hazitavumiliwa,hivyo basi kuwa mstaarabu.Mwenyezi Mungu na akuongoze.Aamin!